Rais Uhuru Kenyatta amekabidhiwa uenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na mwenyekiti anayeondoka, Rais wa Rwanda, Paul Kagame kwenye mkutano wa wakuu wa nchi za jumuiya hiyo ambao ulifanywa kwa njia ya mtandao.
Wakati huo huo, Dkt. Peter Mathuki ambaye ni raia wa Kenya kwa sasa ndiye Katibu Mkuu mpya wa jumuiya hiyo akichukua nafasi ya Balozi Liberate Mfumukeko raia wa Burundi ambaye amekamilisha muhula wake. Kabla ya uteuzi huo, Mathuki alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Biashara la nchi za Afrika Mashariki.
Kwenye mkutano huo, ambao pia ulihudhuriwa na rais Paul Kagame wa Rwanda na Makamu Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, viongozi wa nchi wanachama walisisitiza umuhimu wa kuendelea kushirikiana na kudumisha amani.
Hata hivyo, mmoja wa majaji wapya wa Mahakama ya Haki ya Afrika Mashariki, Kathurima M’Inoti aliapishwa.