Msanii asiyeishiwa na vituko nchini Ringtone Apoko ametoa makata ya siku kwa mungu ampe gari aina BMW i8 la sivyo atachukua maamuzi magumu.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Ringtone amesema iwapo maombi yake hayatajibiwa kwa kipindi cha siku kumi huenda akachukua maamuzi magumu ya kujitoa uhai kwa njia ya sumu.
Kauli hiyo Ringtone imewashangaza wafuasi wake wengi kwenye mitandao ya kijamii ambao wameoneshwa kusikitishwa na tamko la msanii huyo huku wakimtaka aache kufanya mzaha akitumia jina la Mungu.
Ikumbukwe mapema mwaka huu ringtone alitangaza kuwa ataacha muziki wa injili kama mungu atajibu maombi yake ya kumiliki gari aina BMW i8.