Rapa kutoka Marekani Rick Ross kupitia mahojiano yake na Shannon Sharpe kwenye Episode mpya ya 17 ya ‘Club Shay Shay’ ameweka wazi kuwa anapokea mkwanja mrefu kutoka kwa waongozaji na watengenezaji wa filamu kwa kuigiza filamu katika mjengo wake uliopo Fayetteville, Georgia nchini Marekani.
Rick Ross amesema kuwa, anatoza kiasi cha hadi $2.75 Milioni ambazo ni zaidi ya millioni 300 za Kenya kwa baadhi ya vipande vya filamu kuigiziwa katika mjengo wake.