KING KAKA AWATOLEA UVUVI WAWAKILISHI WADI BAADA YA KUPITISHA MSWADA WA BBI

You are currently viewing KING KAKA AWATOLEA UVUVI WAWAKILISHI WADI BAADA YA KUPITISHA MSWADA WA BBI
  • Post category:Burudani

Rapa wa humu nchini King Kaka amewachana wawakilishi wadi kwa hatua ya kupitisha mswada wa marekebisho ya katiba kupitia mpango wa maridhiano ya kitaifa (BBI).

King Kaka anadai kwamba madiwani walipitisha mswada wa BBI kwa sababu rais uhuru kenyatta aliwahidia kuwapa mkopo wa shillingi millioni 2 kununua magari.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram mkali huyo wa ngoma ya “Utanipatia” amewatolea uvivu wawakilishi wadi kwa hatua ya kuisaliti nchi kwa shilllingi millioni 2 ili tu wapasisha mswada wa BBI.

Ikumbukwe King Kaka ni moja kati ya wasanii wanaohisi kuwa kwenye kambi ya Naibu wa Rais William Ruto kwa sababu amekuwa akitumia mitandao yake ya kijamii kuupinga mswada wa marekebisho ya katiba kupitia mapendekezo ya ripoti ya mpango wa maridhiano (BBI).

Robert Elim

Robert Elim better known as Mtoto wa Nyumbani Roba is a new shade of light on the mainstream radio scene! He host an Entertainment show called Interact that usually runs every Monday to Friday from 1:00 PM to 4:00 PM and Interact Extra that runs every Saturday from 10:00 AM to 1:00 PM. Follow him on Twitter and Instagram @robertchiwawa