Suala la kuachia EP, kwa sasa kwenye kiwanda cha muziki nchini, limekuwa likizidi kushamiri na kila msanii amekuwa akionyesha uwezo wake katika kazi zake.
Sasa Msanii Nviiri the Story teller kutoka Sol generatiom ameachia Ep yake mpya iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu na mashabiki zake.
Ep hiyo inayokwenda kwa jina la “Kitenge” imebeba ngoma sita za moto huku akiwa amewashirikisha wasanii kama Sanaipei Tande, Khalighraph Jones na Sauti Sol.
Hata hivyo Kitenge EP iliyotoka chini ya lebo ya muziki ya Sol Generation inayomilikiwa na Sauti Sol inapatikana exclusive kupitia digital platforms zote za kupakua na kusikiliza muziki duniani.