Baby Mama wa Diamond Platinumz Zari Hassan ambaye kwa sasa anaishi nchini Afrika Kusini amemtolea uvivu mtumiaji mmoja wa mtandao wa Instagram aliyetaka kujua anachofikiria kuhusu hatua ya Tanasha Donna kumtembelea Diamond.
Mtumiaji huyo ambaye alishuka kwenye uwanja wa comment ya post ya Zarri Hassan aliandika “ZARI, TANASHA NAE KALETA MTOTO UNAJISKIA AJE UKO ULIPOO?”
Sasa comment hiyo haikupokelewa vyema na Zari Hassan ambaye pia alishuka kwenye uwanja wa comment na kumchana mtumiaji huyo wa Instagram kwa kusema ;“ASANTE KWA UMBEA, WACHA NIJINYONGE. “LEARN TO MIND YOUR BUSINESS. MWANAMME SIYUNA WATOTO WENGI.SMH.”
Kauli hiyo ya Zari Hassan imetafsiriwa na wajuzi wa mambo kuwa huenda mwanamama huyo hajefurahishwa na hatua ya Tanasha Donna pamoja na mtoto wake Naseeb Junior kumtembelea Diamond Platinumz.
Ikumbukwe kwa sasa Tanasha Donna yupo nchini Tanzania ambako ameonekana wakiwa katika mahaba mazito Diamond Platinumz licha ya kuachana mwaka wa 2020 na inadaiwa mrembo huyo amekita kambi nchini humo kwa lengo la kuandaa video yake mpya na msanii wa bongofleva Nandy lakini pia ana mpango wa kukutana na Hamisa Mobeto ambaye wana mpango wa kufanya kazi ya pamoja.