Msanii nyota wa muziki kutoka lebo ya WCB, Rayvanny ameachia rasmi album yake ya kwanza, iitwayo ‘Sound from Africa’.
Rayvanny chini ya lebo hiyo ameachia album hiyo yenye jumla ya nyimbo 23, iliyowashirikisha wasanii kibao wa ndani na nje ya bara la afrika.
Album hiyo imewashirikisha wakali kutoka tanzania, uholanzi, congo, Marekani, Nigeria, Uganda, Msumbiji, Afrika Kusini na Morocco.
Album ya ” Sound from Africa” inapatikana ‘Exclusive’ kupitia mitandao yote ya kukisikiliza na kuuza muziki duniani kama vile Boomplay,Spotify na Apple Music