Mtandao wa Pollstar umetaja orodha ya wasanii weusi ambao wametengeneza pesa ndefu kupitia ziara za muziki (The Highest-Grossing Black Touring Artist) katika kipindi cha miaka 21.
Kwenye orodha hiyo iliyojumuisha Wanamuziki 7, Beyonce ameshika nafasi ya kwanza, akiingiza zaidi ya ($1 Billion) kwenye ziara zake zote za muziki tangu mwaka 2000.
1. Beyonce – Over $1 Billion
2. Jay-Z – $695 Million
3. Drake – $348 Million
4. Rihanna – $336 Million
5. Tina Turner – $235 Million
6. Kanye West – $219 Million
7. Prince – $207 Million