Baada ya uvumi kusambaa mitandoni kuwa msanii kutoka nchini Uganda Jose Chameleone ana mpango wa kumtimua meneja wake Bijoue Fortunate kwa kuzembea kazini.
Sasa meneja huyo amejitokeza na kunyoosha maelezo kuhusiana na suala hilo kwa kusema kuwa bado anafanya kazi na Jose Chameleone.
Akipiga stori na runinga moja nchini Uganda Fortunate amesema kwamba kama kweli Chameleone angekuwa na mpango wa kuvunja mkataba wake angefuata taratibu nzuri za kumfikishia taarifa hizo.
Hata hivyo Jose Chameleone bado yupo kimya juu ya suala hilo ila wajuzi wa mambo wanasema kwamba huenda Fortunate akatimulia kama meneja wa msanii huyo baada ya kutofanikisha malengo yake ya kimuziki.