Mwenyekiti wa Bodi ya Filamu nchini Ezekiel Mutua amefunguka na kueleza sababu za zilizopelekea mchekeshaji wa humu nchini Mulamwah kutopewa wadhfa wa “Ubalozi wa Maudhui Safi” licha ya kuahidiwa wadhfa huo.
Kupitia ukurusa wake wa Twiter, Mutua amesema kuwa mcheshi huyo hakufikia vigezo vya kuwa “Balozi wa Maudhui Safi”, na ndio maana aliachwa nje huku akisema kuwa bodi hiyo haiungi mkono maadhui yanayokwenda kinyume na maadili ya jamii.
Mutua alienda mbali zaidi na kuomba msamaha Mulamwah kwa kutoa ahadi hewa kwake ikizingatiwa kuwa maoni aliyoyatoa yalikuwa mapendekezo yake binafsi wala hayakuwa ya serikali.
Kauli ya Mutua inakuja mara baada ya Mulamwah kuibua tweet yake ya zamani aliyomhaidi nafasi ya Ubalozi wa maudhui safi,ahadi aliyosema hajatimiza hadi sasa.