Rapa kutoka Nchini marekani Tekashi 69 ameweka wazi kuwa sababu zilizompelekea asifanye muziki na kuacha kutumia mtandao wa Instagram kwa muda miezi 6 ni kuongezeka uzito (Kunenepa) hivyo alitaka kujizingatia yeye mwenyewe kwanza.
Tekashi ameielezea sababu hiyo kupitia ukurasa wake wa Instagram kwa kuandika alijikuta kibonge kutokana na kupenda kula kula hali iyopelekea kunenepa na kuongezeka Uzito na kufikisha zaidi kilo 90.
Hata hivyo amesema amefanikiwa kupunguza zaidi ya kilo 20, na anaufurahia mwonekano wake wa sasa.