Zikiwa ni Siku chache tu baada ya kuachiwa huru kwa msamaha wa rais Trump, Rapa wa Florida Kodak Black ameamua kusherehekea uhuru wake kwa kuachia Ngoma mpya iitwayo ‘Last day in’
Katika Ngoma hiyo Kodak anagusia kuachiliwa kwake kutoka gereza la shirikisho nje ya Chicago Jumatano iliyopita baada ya kutumikia karibu nusu ya kifungo chake cha miezi 46 kwa kosa la kudanganya nyaraka ya kupata bunduki.
Kodak pamoja na Lil Wayne na Mkurugenzi Mtendaji wa Roc Nation, Desiree Perez ni miongoni mwa watu 145 walionufaika na msamaha na mabadiliko ya vifungo yaliyotolewa na Donald Trump siku yake ya mwisho ofisini kabla Rais Mpya Joe Biden hajaapishwa