Msanii nguli wa muziki wa Hiphop kutoka Uganda GNL Zamba ameweka wazi kuwa hakuna rapa yoyote kwa sasa nchini humo anayemfanya ashindwe kulala usiku akimsikiliza.
Akiwa kwenye moja ya Interview GNL Zamba ambaye vizuri na wimbo wake uitwao “Saba Saba” amesema marapa wengi nchini Uganda wamepoteza uhalisia wa muziki wa hiphop kwani mashairi yao hayaendani na midundo ya nyimbo husika, jambo ambalo anadai imepelekea muziki wao kukosa mashiko.
GNL Zamba ambaye ni moja kati ya wasanii nguli wa muziki wa hiphop nchini Uganda amekuwa akiwasifia wasanii Fefe Bussi, Navio, na Recho Ray huku kwa upande mwingine akionekana kuwarushia madongo wasanii Gravity Omuttujju na Victor Kamenyo ambao wamekuwa wakishandane nae kwenye muziki wa Hiphop.