Kundi la muziki wa rap nchini Tanzania Weusi wameachia rasmi album yao inayokwenda kwa jina la “Air Weusi.”
Air Weusi ina jumla ya nyimbo 14, ikiwa na kolabo 2 pekee waliyomshirikisha Khadija Kopa na nyingine wamemshirikisha Big boss Jojo.
Waandaaji wa muziki waliohusika kuikamilisha album hiyo ni watano tuu akiwemo Luffa, S2kizzy, Nahreel na wengine huku mixing na mastering zikiwa zimesimamiwa na Chizan Brain .
Tayari album hiyo inapatikana kupitia majukwaa yote ya kusikiliza muziki (digital platform).