Rapa kutoka nchini Uganda GNL Zamba aligonga vichwa vya habari vya burudani majuzi mara baada ya kutangaza kwamba anamtafuta mke wa pili afunge nae ndoa.
Zamba kwenye interviews mbali alikiri kwamba mke wake Tamar ambaye ni raia wa nchini marekani alimpa ruhusa ya kumuoa mke wa pili kutoka Africa.
Sasa rapa huyo kwenye moja ya Interview ametengua kauli yake hiyo ya kumuoa mke wa pili kwa kusema kwamba alikuwa anatania tu, hivyo watu wasichukulie jambo kwa ukubwa.
Hata hivyo GNL Zamba amewataka wanawake ambao wamekuwa wakimtumia picha zao kwenye mitandao yake ya kijamii kwa ajili ya kumshawishi wafunge nae ndoa wakome mara moja kwani anamheshimu mke wake.