Msanii nguli wa muziki wa hipop nchini marekani Jay-Z ni mwingi wa kutoa na ndio maana anaongezewa zaidi, sasa rapa huyo ameahidi kuchangia nusu ya malipo yake kutoka kwenye wimbo wa “What It Feels Like” kwenda kwa familia ya marehemu Nipsey Hussle.
Baada ya kutoka kwa wimbo huo ambao ameshirikiana na Nipsey Hussle, Jay-Z amezungumza na jarida la GQ na kusema kiasi alicholipwa na waandaaji wa filamu ya ‘Judas and the Black Messiah’ hivyo atatoa nusu ya pesa hizo kwenda kwa familia ya Nipsey lakini pia nusu nyingine ataipatia familia ya Fred Hampton, ambaye alikuwa mwanaharakati na kiongozi wa chama cha Black Panther ambaye aliuawa mwaka wa 1969.