Staa wa muziki wa Hiphop kutoka nchini Marekani DaBaby amefunguliwa mashtaka kwa kosa la kumpiga ngumi mwenye nyumba hadi kumtoa Jino.
Rapa huyo alikodisha nyumba kwa ajili ya kufanyia video ya wimbo wake, na walikubaliana na mwenye nyumba kuwaingiza watu 12 tu ndani kulingana na kanuni za COVID-19.
Kinyume na masharti, DaBaby aliingiza watu takribani 40, mwenye nyumba hiyo ambaye amefahamika kwa jina la Gary Pagar alipoamua kumfuata kwa kuvunja masharti ya mkataba, mtu mmoja kutoka kambi ya DaBaby alimvamia na kumuangusha chini.
Baada ya hapo DaBaby alitoka kwenye gari na kumkimbiza pagar hadi ndani ambapo alianza kwa kumuonya kutowapa taarifa polisi kisha alimtwanga ngumi ya uso hadi kumng’oa jino. Shuhuda mmoja alipiga simu kuita polisi, na DaBaby na timu yake walikimbia eneo hilo.