RAYVANNY AMUOMBA RADHI KAJALA NA WOTE WALIOKWAZWA NA VIDEO ALIYOWEKA MTANDAONI.

You are currently viewing RAYVANNY AMUOMBA RADHI KAJALA NA WOTE WALIOKWAZWA NA VIDEO ALIYOWEKA MTANDAONI.
  • Post category:Burudani

Nyota wa muziki kutokea lebo ya WCB Wasafi, Rayvanny amemuomba radhi mwigizaji wa Bongo Movie Fridah Kajala kwa video aliyoshare mtandaoni akiwa katika hali ya mahaba na binti wa mwigizai huyo, Paula.

Rayvanny alichukua hatua hiyo kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo pia aliwaomba radhi wazazi na watu wote ambao kwa namna yoyote walikwazwa na video hiyo mtandaoni wiki kadhaa zilizopita.

Kauli hiyo ya Rayvanny inakuja mwezi mmoja mara baada ya kupost video kwenye ukurasa wake wa Instagram isiyo na maadili kwenye jamii akiwa na binti ya mwigizaji wa bongo Movie Fridah Kajala, Jambo ambalo liliibua hisia mseto miongoni mwa wadau wa muziki wa Bongofleva wengi wakioneka kukemea tukio hilo.

Robert Elim

Robert Elim better known as Mtoto wa Nyumbani Roba is a new shade of light on the mainstream radio scene! He host an Entertainment show called Interact that usually runs every Monday to Friday from 1:00 PM to 4:00 PM and Interact Extra that runs every Saturday from 10:00 AM to 1:00 PM. Follow him on Twitter and Instagram @robertchiwawa