Klabu ya Paris Saint-Germain ya nchini Ufaransa wamepanga kumpa Lionel Messi mshara wa pauni 800,000 kwa wiki kama mchezaji huyo atajiunga na kikosi hicho kilichopania kufanya makubwa msimu ujao (2021-2022).
Mkataba wa Messi na Barcelona unatarajiwa kumalizika mwezi Juni mwaka huu ndio maana PSG wameweka nguvu nyingi kumpata mchezaji huyo.
Hata hivyo PSG itapata upinzani mkubwa kutoka kwa timu ya Manchester City ambayo pia inamuwinda nyota huyo, lakini kulingana na mtandao wa Sportsmole wa nchini Uingereza, PSG wametangaza ofa hiyo kubwa kwa lengo la kumshawishi aweze kutua katika timu yao.
PSG YAMUANDALIA LIONEL MESSI KITITA CHA MSHAHARA.
