Klabu ya FC Bournemouth imetajwa kuwa kwenye mazungumzo na Thierry Henry kwa ajili ya kuja kuifundisha timu hiyo inayoshiriki ligi ya Championship nchini England.
Nyota huyo wa zamani wa Arsenal aliwahi kuifundisha Klabu ya AS Monaco inayoshiriki Ligi Kuu nchini Ufaransa, kwa sasa anaifundisha Klabu ya CF Montrèal ambayo inashiriki Ligi Kuu nchini Marekani maarufu kama MLS.