Michezo miwili itapigwa leo kati ya Borussia Mönchengladbach dhidi ya Manchester city huku Atalanta ikiialika Real Madrid.
Kiwango bora walichonacho Manchester City katika mashindano ya ndani kinakwenda kujaribiwa usiku wa leo kwenye Uwanja wa Puskas.
Uwanja wa Puskas unatumika kama eneo la nyumbani kwa Gladbach kwa sababu ya vizuizi vya Serikali ya Ujerumani ambavyo vinakataza timu ya kigeni kuingia Nchini humo.