PATRICE MOTSEPE ATANGAZWA KUWA RAIS MPYA CAF

You are currently viewing PATRICE MOTSEPE ATANGAZWA KUWA RAIS MPYA CAF
  • Post category:Michezo

Bilionea wa Afrika Kusini na Mmiliki wa klabu ya Mamelod Sundowns ya Afrika Kusini, Patrice Motsepe amechaguliwa kuwa Rais wa saba wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF).

Patrice amechaguliwa kwenye uchaguzi uliofanyika Ijumaa (Machi 12, 2021) huko Morocco kwenye mkutano mkuu wa CAF.

Motsepe alizaliwa Januari 28, 1962 huko Pretoria, Afrika Kusini. Ana mke na watoto watatu na makazi yake yako Johannesburg, Afrika Kusini.

Kwa mujibu wa Mtandao wa Forbes, Motsepe ana utajiri wa Dola 3 bilioni unaomfanya ashike nafasi ya tisa katika orodha ya matajiri barani Afrika huku kidunia akiwa nafasi ya 1513.

Chanzo kikuu cha utajiri wake ni biashara ya madini na uwekezaji katika sekta nyingine alioufanya.

Katika soka, Motsepe anafahamika kwa umiliki wake wa klabu ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini ambayo aliinunua mwaka 2003.

Robert Elim

Robert Elim better known as Mtoto wa Nyumbani Roba is a new shade of light on the mainstream radio scene! He host an Entertainment show called Interact that usually runs every Monday to Friday from 1:00 PM to 4:00 PM and Interact Extra that runs every Saturday from 10:00 AM to 1:00 PM. Follow him on Twitter and Instagram @robertchiwawa