Ni Rasmi klabu ya Manchester United imemruhusu mchezaji wake muargentina Marcos Rojo kutoka klabuni hapo na kujiunga klabu ya Boca Juniors ya huko kwao Argentina.
Rojo amejiunga na Boca Juniors kwa uhamisho huru baada ya United kusitisha mkataba wake ambao ulitakiwa kuisha mwezi Juni mwaka wa 2021 na kumruhusu Rojo kujiunga na miamba hiyo ya soka nchini Argentina.
Licha ya kiwango chake kuwa kizuri lakini hajapata muda mwingi wa kucheza klabuni hapo kwa sababu ya kuandamwa na majeraha ya mara kwa mara.