FIFA YAZINDUA TAWI LA MAENDELEO YA SOKA RWANDA.

You are currently viewing FIFA YAZINDUA TAWI LA MAENDELEO YA SOKA RWANDA.
  • Post category:Michezo

Raisi wa Shirikisho la mpira wa miguu duniani, FIFA, Gianni Infantino amezindua rasmi tawi la sgirikisho hilo katika mji mkuu wa Rwanda Kigali.

Makao makuu ya tawi hilo la FIFA la maendeleo ya mpira wa miguu katika eneo hili la Afrika yalikuwa nchini Ethiopia, lakini baadae FIFA ikaamua kuyahamishia mjini Kigali.

Katika uzinduzi huo uliofanyika katikati mwa mji wa Kigali, Bwana Gianni Infantino aliambatana na wenyeji wake, Waziri wa mambo ya nje Vincent Biruta pamoja na Waziri wa michezo Aurore Munyangaju.

Kulingana FIFA tawi hilo litakuwa na jukumu la kuhakikisha maendeleo ya mpira wa miguu yanafikiwa katika maeneo ya Afrika Mashariki na kati.

Pia litakuwa na jukumu la kupokea mikutano ya wajumbe wa FIFA katika eneo hilo na kutoa ushauri na taarifa kuhusu soka ya eneo hilo kwenye makao makuu ya FIFA yaliyoko Zurich nchini Uswiss.

Robert Elim

Robert Elim better known as Mtoto wa Nyumbani Roba is a new shade of light on the mainstream radio scene! He host an Entertainment show called Interact that usually runs every Monday to Friday from 1:00 PM to 4:00 PM and Interact Extra that runs every Saturday from 10:00 AM to 1:00 PM. Follow him on Twitter and Instagram @robertchiwawa