Beki wa Real Madrid Mbrazili Marcelo da Silva huenda akaungana tena na Cristiano Ronaldo baada ya Juventus kuonesha nia ya kutaka kumsajili.
Marcelo amekuwa sehemu kubwa ya mafanikio ya Madrid tangu atue klabuni hapo mwaka 2016 lakini kwa sasa nafasi yake imechukuliwa na Ferland Mendy kitu kinachomfanya kutaka kuondoka Hispania mwishoni mwa msimu huu kumalizika.