Baada ya kupata sare mbili za bila kufungana dhidi ya Real Sociedad kisha na Chelsea, Manchester United inasafiri hii leo kuelekea Selhurst kukipiga dhidi ya Crystal Palace mchezo utaopigwa saa 5 usiku kwa saa za Afrika Mashariki.
Katika mchezo huo Kocha wa United, Ole Gunnar Solskjaer anatarajia kuwakosa wachezaji wake wawili muhimu ambao ni Paul Pogba na Phil Jones.
Michezo mingine itakayopigwa leo ni kati ya Burnley dhidi ya Leicester City na Sheffield United dhidi ya Aston Villa, saa tatu usiku.