Kocha wa Timu ya Taifa ya Soka ya Wanaume ya Ujerumani, Joachiam Low ataacha kuifundisha timu hiyo baada ya Michuano ya EURO inayotarajiwa kufanyika Juni 11 – July 11, mwaka wa 2021.
Chama cha Soka cha Ujerumani (DFB) kimesema, mkataba wa Low ulitakiwa kuisha baada ya Michuano ya Kombe la Dunia 2022 ila Kocha huyo ameomba kusitisha mapema mkataba.
Low aliiwezesha Ujerumani kushinda Kombe la Dunia 2014 huko Brazil, alianza kuinoa timu hiyo mwaka 2006 baada ya kuwa kama Msaidizi wa Jürgen Klinsmann katika timu hiyo.
Kwa siku za karibuni, Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp amekuwa akipigiwa upatu kumrithi Low kuinoa timu hiyo ingawa Klopp mwenyewe amekanusha taarifa hizo na kusema mbeleni inawezekana ila si kwa sasa.