Washambuliaji, Zlatan Ibrahimovic na Romelu Lukaku wamepewa adhabu ya kufungiwa mchezo mmoja wa Ligi Kuu Italia kufuatiwa kuanzisha vurugu katika mchezo wa ‘Derby ya Milan’ uliopigwa Jumanne iliyopita.
Ibrahimovic atakosa mchezo mmoja baada ya kuonyeshwa kadi mbili za njano moja ya kadi hizo ni baada ya kuanzisha vurugu dhidi ya Lukaku.
Lukaku alipewa kadi ya njano ya pili baada ya kupata kadi nyingine katika mchezo wa nyuma wa kombe la Coppa Italia.