PRODYUZA WASHINGTON AKANA MADAI YA KUHUSIKA KWENYE MAUJI YA MSANII MOZEY RADIO.

You are currently viewing PRODYUZA WASHINGTON AKANA MADAI YA KUHUSIKA KWENYE MAUJI YA MSANII MOZEY RADIO.
  • Post category:Burudani

Prodyuza muziki nchini Uganda Washington amekana madai yanayosambaa mitandao kuwa alihusika kwenye mauaji ya mwanamuziki Mozey Radio.

Hii ni baada ya, Boomlocks  ambaye ni ndugu wa msanii Peter Miles kujitokeza na kudai kwamba Washington alihusika kwenye wa mauji ya msanii Mozey Radio kwani kabla ya umauti kumkuta msanii huyo alikuwa nae kwenye viwanja vya kukulia bata.

Sasa akiwa kwenye moja ya interwiew pdodyuza washington amepuuzilia mbali madai ya Boomlocks na kusema kwamba anatumia jina lake kutafuta umaarufu.

Sanjari hilo inadaiwa kuwa Baby Mama wa msanii mozey Radio, Lilian Mbabazi amefungua tena kesi ya mauaji ya msanii huyo huku akitaka uchunguzi zaidi kufanya ili kubaini chanzo cha  mauaji ya Mozey Radio.

Ikumbukwe Mozey Radio alifariki mwaka wa 2018 baada ya kupata majeraha mbaya ya kichwa aliposhambuliwa akiwa kwenye bar moja huko Entebbe Uganda. Lakini mwaka wa 2019 mahakama nchini Uganda  ilitoa hukumu ya miaka 13 jela  kwa mshukiwa mkuu wa mauji ya Mozey Radio aitwaye Godfrey Wamala baada ya kukiri kumuua msanii huyo.

Robert Elim

Robert Elim better known as Mtoto wa Nyumbani Roba is a new shade of light on the mainstream radio scene! He host an Entertainment show called Interact that usually runs every Monday to Friday from 1:00 PM to 4:00 PM and Interact Extra that runs every Saturday from 10:00 AM to 1:00 PM. Follow him on Twitter and Instagram @robertchiwawa