Msanii nguli wa muziki nchini Mejja ametia neno kuhusu ishu ya wimbo wake wa Siskii kutoingia kwenye trending za mtandao wa Youtube.
Kupitia Ukurasa wake wa Instagram Mejja amesema anahisi kwamba kuna mchezo mchafu unafanyiwa channel yake ya Youtube kuzuia ngoma yake ya siskiii kuingia kwenye video zinazofanya vizuri kwenye mtandao wa youtube huku akisema suala hilo halitamzuia kutoa muziki mzuri.
Kauli ya Mejja inakuja mara baada ya mashabiki zake kuibua mjadala mzito kwenye mtandao wa Twitter, ni kwanini wimbo mpya wa Mejja uitwao “Siskii” haujengia kwenye trending za youtube licha ya ngoma hiyo kuwa kali.
“Siskii” ni wimbo wa pili kutoka kwa Mejja kwa mwaka huu wa 2021 baada ya “Ulimu wangu” uliotoka wiki kadhaa zilizopita na unazidi kufanya vizuri kwenye mtandao wa youtube kwani ina zaidi ya viewers laki tatu ndani ya siku nne tangu kuachiwa kwake.