Ikiwa zimesalia siku chache tuikaribishe siku ya Valentines, Staa wa muziki nchini Uganda Lydia Jazmine ameripotiwa kuachana na mchumba wake wa siku nyingi Fik Fameica.
Duru zinasema baada ya wawili hao kuachana lydia jazmine aliingia studio na kurekodi ngoma mpya iitwayo “I love you bae” mahususi kwa ajili ya mpenzi wake mpya.
Chanzo cha karibu na Lydia Jazmine kimeuambia mtandao Cycone Times kwamba msanii huyo ameachana na fik fameica na kuingia kwenye mahusiano ya kimapenzi na jamaa mmoja tajiri nchini uganda.
Ikumbukwe Lydia jazmine na Fik Fameica wamekuwa kwenye mahusiano kwa muda mrefu ingawa wamekuwa wakikana kwenye vyombo vya habari kuwa hawana uhusiano wowote wa kimapenzi.