LEXSIL AIGURA LEBO YA MUZIKI YA JUST IN LOVE INAYOMILIKIWA NA MSANII OTILE BROWN.

You are currently viewing LEXSIL AIGURA LEBO YA MUZIKI YA JUST IN LOVE INAYOMILIKIWA NA MSANII OTILE BROWN.
  • Post category:Burudani

Mwanamuziki anayefanya vizuri kwenye kiwanda cha muziki nchini Lexsil ameigura lebo ya muziki ya “Just In Love” ikiwa ni miezi 6 tangu ajiunge na lebo hiyo.

Duru zinasema msanii huyo ¬†alivunja mkataba na lebo ya “Just In Love” baada ya kuwepo na makubaliano kati yake na uongozi wa lebo hiyo, hivyo anafanya muziki kama msanii wa kujitegemea.

Taarifa za kuondoka kwa Lexsil zimethibitisha na mmoja wa wasimamizi wa lebo ya “Just In Love” anayefahamika kwa jina la Noriega Don.

Ikumbukwe Lexsil alisainiwa na otile brown kwenye lebo ya “Just In Love” mwezi Septemba mwaka wa 2020 na alifanikiwa kuachia ngoma mbili ambazo ni Dance Along na Remedy aliyomshirikisha Otile Brown.

Kusainiwa kwa Lexsil kulikuja mara baada ya msanii Jovial kuigura lebo ya “Just In Love” kutokana na mgogoro ulioibuka kati yake na Otile Brown ambaye ni mmiliki wa lebo hiyo.

Robert Elim

Robert Elim better known as Mtoto wa Nyumbani Roba is a new shade of light on the mainstream radio scene! He host an Entertainment show called Interact that usually runs every Monday to Friday from 1:00 PM to 4:00 PM and Interact Extra that runs every Saturday from 10:00 AM to 1:00 PM. Follow him on Twitter and Instagram @robertchiwawa