RAPA ZLATAN IBILE ACHORA TATOO MPYA YA RAIS WA ZAMANI WA GHANA “KWAME NKRUMAH”.

You are currently viewing RAPA ZLATAN IBILE ACHORA TATOO MPYA YA RAIS WA ZAMANI WA GHANA “KWAME NKRUMAH”.
  • Post category:Burudani

Rapa kutoka nchini Nigeria Zlatan Ibile ametuonyesha tattoo yake mpya ambayo inaonyesha picha ya mwanasiasa,mwanamapinduzi na aliyewahi kuwa raisi wa nchini Ghana, Kwame Nkrumah.

Kupitia akaunti yake ya instagram Zlatan Ibile amepost picha akiwa kifua wazi huku tattoo hiyo ikionekana maeneo ya kifuani na kuandika “Dr kwame Nkrumah ❤️ ????????” .

Kwa kuzingatia harakati za Nkwame Nkrumah watu wanaweza kudhani rapaZlatan Ibile amechora tattoo hiyo ya sura ya Kwame anamaaanisha kuwa yeye ni mpiganaji wa mapinduzi kama alivYokuwa Kwame Nkrumah.

Kwame Nkrumah alikuwa mwanasiasa na mwanamapinduzi wa Ghana. Alikuwa mratibu wa harakati za Pan-Afrika lakini pia alikuwa Waziri Mkuu wa kwanza na Rais wa Ghana. Aliongoza Gold Coast (ambayo sasa inaitwa Ghana) kupata uhuru kutoka kwa Uingereza mnamo 1957.

Robert Elim

Robert Elim better known as Mtoto wa Nyumbani Roba is a new shade of light on the mainstream radio scene! He host an Entertainment show called Interact that usually runs every Monday to Friday from 1:00 PM to 4:00 PM and Interact Extra that runs every Saturday from 10:00 AM to 1:00 PM. Follow him on Twitter and Instagram @robertchiwawa