Aliyewahi kuwa kocha mkuu wa klabu ya Simba ya Tanzania, Patrick Aussems ametambulishwa rasmi kuwa kocha mkuu wa klabu ya AFC Leopards ya Kenya.
Aussems anajiunga na klabu hiyo baada ya kufanikiwa kuiongoza Simba kutwaa taji la Ligi Kuu ya Tanzania msimu wa 2018/19 na kufika hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa ya Afrika.
Mbeligiji huyo mwenye umri wa miaka 55 ataanza rasmi mazoezi yake ya kwanza leo Jumanne na atasimamia mechi ya kwanza siku Jumamosi kati ya Leopards dhidi ya Taita Taveta All Stars.