Taarifa kutoka katika mtandao wa ‘Express’ umeripoti kuwa Manchester United ipo katika mpango wa kumpa mkataba mpya Bruno Fernandes ili kubakia klabuni hapo.
Fernandes amekuwa katika kiwango bora tangu atue klabuni hapo akitokea Sporting Lisbon ya Ureno msimu uliopita.
Hadi sasa Fernandes ametupia mabao 18 kwenye mashindano yote msimu huu akiwa na magoli mengi zaidi kuliko mchezaji yeyote katika kikosi hicho kinachonolewa na Ole Gunnar Solskjaer.