Mabingwa watetezi wa Ligi kuu nchini Gor Mahia watashuka uwanjani Kasarani Jumapili Februari 7 kwa mechi ya ligi kuu maarufu kama Mashemeji Derby huku kwa mara ya kwanza mechi ya hiyo ya ubabe na utani mkubwa ikichezwa bila mashabiki uwanjani kutoka na ugonjwa wa Covid 19.
Timu zote mbili zilikuwa zimewasilisha ombi kwa wizara ya afya kuruhusu angalau mashabiki 5,000 ila ombi hilo lilikataliwa na kuwalazimu mashabiki kusalia nyumbani wakati wa mchuano huo siku ya Jumapili .
Klabu ya FC Leopards ni ya 4 kwenye msimamo wa ligi nchini kwa pointi 18 wakati Gor Mahia ikishikilia nafasi ya 6 kwa alama 15.