Nyota wa muziki nchini Otile Brown na aliyekuwa meneja wake Dr. Eddie wamemaliza tofauti zao baada ya kutokuwa na maelewano mazuri kwa muda.
Taarifa hizo zimethibitishwa na Dr. Eddie kupitia ukurasa wake wa Instagram baada ya kupost kipande cha video wakiwa location na Otile Brown na kuthibitisha kwamba wanatayarisha video mpya ya msanii huyo.
Dr. Eddie alienda mbali zaidi na kusema kwamba ilibidi wamalize tofauti zao kwa sababu ilikuwa kizingiti kwao kufanya muziki mzuri ambao walikuwa wakifanya miaka ya hapo nyuma.
Ikumbukwe mwaka wa 2017 Otile Brown alitengana na lebo ya muziki ya dream land music chini ya uongozi wake Dr. Eddie, jambo ambalo lilimfanya akawa msanii wa kujitegemea.
Kipindi hicho mkali huyo wa ngoma ya Dusuma, alisema kwamba kilichompelekea kutemana na lebo ya muziki ya Dream Land ni kwa sababu Dr. Eddie alikwenda kinyume na mkataba wa maelewano.
Kitu ambacho kilimfanya Dr. Eddie kumzuia Otile Brown kutumia nyimbo alizorekodi chini ya lebo yake ya muziki kwenye matamasha mbali mbali ya muziki. Lakini sasa inaonekana mambo yamekuwa mazuri, hivyo wawili hao wameahamu kufanya kazi tena.