Aliyekuwa mwigizaji wa kipindi cha “Tahidi high” Joseph Kinuthia maarufu kama Omosh ametoa ujumbe wa shukran kuwapongeza Wakenya ambao wanaendelea kujitokeza na kumsaidia baada ya kuona magumu aliyokuwa anapitia katika maisha kwenye video iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii.
Kupitia video aliyoshare kwenye mitandao yake ya kijamii Omosh amesema amefurahia upendo ambao amepokea kutoka kwa wakenya huku pia akimpongeza mchekashaji wa humu nchini Jalang’o ambaye tayari amechangisha zaidi ya shillingi millioni moja za kumsaidia kimaisha.
Katika video nyingine mwigizaji huyo amedokeza kwamba amepewa ardhi ya bure pamoja na mifuko 50 ya simiti na kampuni ya Zero Hero Properties kwa ajili ya ujenzi wa nyumba yake.