OMBI LA BOB WINE KUONDOA KESI YA UCHAGUZI LAAHIRISHWA

You are currently viewing OMBI LA BOB WINE KUONDOA KESI YA UCHAGUZI LAAHIRISHWA

Mahakama ya juu nchini Uganda imeahirisha ombi la Robert Kyagulanyi maarufu kama Bobi Wine la kuondoa kesi aliyowasilisha kupinga matokeo ya uchaguzi mkuu wa rais mwaka 2021.

Tume ya Uchaguzi ilimtangaza mshindi Rais Museveni wa chama cha NRM kwa aslimia 59% huku Kyagulanyi akipata asilimia 35.

Kesi hiyo imeahirishwa kufuatia ombi la mawakili wa Robert Kyagulanyi kwamba leseni yao ya kazi imemalizika tarehe 28 mwezi wa Februari mwaka 2021.

Jaji mkuu wa Uganda Alfonse Owiny Dollo anayeongoza Japo la majaji tisa amempatia wakili wa Kyagulanyi, Merdard Ssegona Lubega hadi saa kumi na moja leo awe amepata leni yake kutoka kwa msajili wa mahakama.

Kesi hiyo itaendelea kesho Ijumaa saa tatu na nusu asubuhi ambapo mahakama kuu inatarajiwa kutoa uamuzi wa ombi la Bobi Wine kuondoa kesi.

Robert Elim

Robert Elim better known as Mtoto wa Nyumbani Roba is a new shade of light on the mainstream radio scene! He host an Entertainment show called Interact that usually runs every Monday to Friday from 1:00 PM to 4:00 PM and Interact Extra that runs every Saturday from 10:00 AM to 1:00 PM. Follow him on Twitter and Instagram @robertchiwawa