Mwimbaji kutoka nchini Nigeria Omah Lay ameweka wazi kuibiwa vitu vyake akiwa uwanja wa ndege huku msanii huyo akiwa anajiuliza kama waliomuibia vitu hivyo walikuwa wanataka nyimbo zake ambazo hazijatoka au kitu gani.
Omah Lay ametoa taarifa hiyo kupitia ukurasa wake wa Twitter kwa kuandika “Nimeibiwa laptop,Microphone na Audio interface kutoka kwenye box langu uwanja wa ndege,nyinyi watu mlikuwa mnatafuta hit song au kitu gani?”
Omah Lay hajaweka wazi moja kwa moja ni uwanja gani wa ndege ambao ameibiwa vitu hivyo lakini pia hajaweka wazi tukio hilo lilitokea lini.