Msanii nguli wa muziki kutoka nchini Uganda Jose Chameolene amedai kwamba kura zake kwenye kinyanganyiro cha umeya wa jiji la Kampala zilikumbwa na dosari nyingi.
Akiwa kwenye moja ya Interview Chameleone amesema kura zake ziliaharibiwa na baadhi ya wagombea waliojitokeza kuwania wadhfa huo ambao waliogopa umaarufu wake.
Hata hivyo amedokeza mpango wa kurejea tena kwenye kiwanda cha muziki nchini Uganda kwa kishindo lakini pia amedai kwamba ataelekeza nguvu zake zote kuboresha kituo chake cha runinga kiitwacho Leone Island TV.
Ikumbukwe Jose Chameolene alipoteza kwenye uchaguzi wa umeya wa jiji la Kampala mapema mwaka huu na mpinzani wake Erias Lukwago.