Msaani wa muziki asiyeishiwa na vituko nchini Ringtone Apoko amefunguka sababu za kumshinikiza Mungu ampe gari aina BMW i 8.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Ringtone amesema kuwa anataka kuwaonyesha wanamuziki wa kidunia kuwa hawana pesa, na hivyo wamrudie mungu kwa sababu yeye ndiye muweza yote.
Kauli ya Ringtone inakuja siku chache baada ya kuibua hisia mseto miongoni mwa wafuasi wake aliposema kuwa ataacha muziki wa injili kama maombi yake hayatajibiwa.
Ikumbukwe mapema mwezi januari mwaka huu ringtone alitangaza kufunga kwa siku 40 kwa lengo la kumuomba mungu ampe gari aina BMW i8.