TUZO ZA GRAMMY 2021 KUFANYIKA JUMAPILI HII

You are currently viewing TUZO ZA GRAMMY 2021 KUFANYIKA JUMAPILI HII
  • Post category:Burudani

Tuzo za Grammy mwaka 2021 zinatarajiwa kufanyika Jumapili hii Machi 14, Hafla ya Tuzo hizo za 63 itafanyika Huko Los Angeles, nchini Marekani huku Mastaa kama Cardi B, Megan Thee Stallion na Lil Baby wakitarajiwa kudondosha Burudani wakati wa hafla hiyo inayosubiriwa kwa hamu kote Duniani.

Roddy Ricch , BTS ,Post Malone, Doja Cat, DaBaby, Taylor Swift, na Billie Eilish pia watatumbuiza wakati wa sherehe hiyo, ambayo itazingatia miongozo ya usalama wa COVID-19.

Katika Tuzo za Grammy 2021 Beyoncé ndiye Msanii aliyeteuliwa katika Vipengele vingi zaidi  akiwa ameteuliwa kwenye vipengele 9 , akifuatiwa na Taylor Swift, Dua Lipa, na Roddy Ricch Vipengele sita kila mmoja.

The African Giant, Burnaboy pia ni miongoni mwa wasanii wanaowania Tuzo za Grammy 2021 katika Kipengele ‘Best Global Music Album’.

Tuzo za Grammy za 2021 awali zilipangwa kufanyika mwezi Januari kabla ya kuahirishwa hadi Machi kwa sababu ya ongezeko la maambukizi ya COVID-19 huko Los Angeles.

Robert Elim

Robert Elim better known as Mtoto wa Nyumbani Roba is a new shade of light on the mainstream radio scene! He host an Entertainment show called Interact that usually runs every Monday to Friday from 1:00 PM to 4:00 PM and Interact Extra that runs every Saturday from 10:00 AM to 1:00 PM. Follow him on Twitter and Instagram @robertchiwawa