NDOA YA KANYE WEST NA MKEWE KIM KARDASHIAN IMECHUKUA SURA MPYA.

You are currently viewing NDOA YA KANYE WEST NA MKEWE KIM KARDASHIAN IMECHUKUA SURA MPYA.
  • Post category:Burudani

Staa wa vipindi vya Keeping Up with the Kardashians, mrembo Kim Kardashian bado hajaomba talaka kutoka kwa mumewe Kanye West ambaye alishaachana nae.

Kwa mujibu wa mtandao wa E Online, chanzo cha karibu na Kim Kardashian, kimeuambia mtandoa huo kuwa kilichobaki kwa sasa nikusubiri utaratibu tu.

Chanzo hicho pia kimeongeza kwamba, Kim kardashian na Kanye West wamemalizana kabisa na hawazungumzi tena. 
Ingawa watu wengi wanajua hali ya uhusiano wa Kim Kardashian na

Kanye West kwa sasa ulivyo, chanzo hicho kinaelezea kwamba Kim bado hajaanzisha shughuli rasmi ya kufuatilia talaka kwa sababu, Bado anashughulikia jinsi atakavyo tangaza talaka hiyo.

Sanjari na hilo, chanzo cha pili upande wa Kanye West, pia kiliuambia mtandao wa E Online kuwa, Kanye West pia amemalizana kabisa na ndoa na anaendelea na maisha yake.

Robert Elim

Robert Elim better known as Mtoto wa Nyumbani Roba is a new shade of light on the mainstream radio scene! He host an Entertainment show called Interact that usually runs every Monday to Friday from 1:00 PM to 4:00 PM and Interact Extra that runs every Saturday from 10:00 AM to 1:00 PM. Follow him on Twitter and Instagram @robertchiwawa