Mwanamuziki wa bongo fleva, ‘Nandy’ amesema kuwa watu wengi wana hofu kwamba huenda akawa mjazito lakini ukweli ni kwamba hana mimba.
Nandy ambaye anafanya vizuri na wimbo wake wa “Leo Leo” amesema kuwa ameshapata maswali mengi kuhusiana na tumbo lake baada ya kuweka picha ya mwanamke mjamzito kwenye profile yake ya mtandao wa whatsapp, hivyo kupokea maswali mengi kuhusiana na hilo.
Hata hivyo mrembo huyo ambaye yupo kwenye mahusiano ya kimapenzi na Billnas amekanusha taarifa za kuachana na mpenzi wake huyo ambaye ni mwanamuziki wa Bongo fleva.