Rapa kutoka nchini Uganda Navio amewarai wadau wa muziki nchini humo kutozuzia tuzo za MTV Africa Music Awards zitakazofanyika tarehe 20 mwezi huu.
Akiwa kwenye moja ya interview Navio amewataka wa ganda kutoingiza siasa kwenye masuala ya burudani ikizingatiwa kuwa tuzo hizo zinafanyika kwa mara ya kwanza nchini Uganda.
Aidha amesema iwapo wadau wa muziki watasusia tuzo hizo, wanamuziki wataathirika kiuchumi kwani tuzo za MTV Africa Music Awards zitatoa nafasi kwa wasanii wenye vipaji kuonyesha uwezo wao kwenye muziki.
Kauli inakuja baada ya kuwepo kwa ripoti kuwa baadhi ya wadau wa muziki nchini Uganda wanapanga kususia tuzo za MTV Africa Music Awards kwa madai kuwa tuzo hizo zina upendeleo kwa baadhi ya wanamuziki wa zamani.