Mwanamuziki kutoka nchini Uganda Eezy amefunguka sababu za kuchelewa kuachia remix ya wimbo wake wa”Tumbiza Sound” licha ya kuwepo na mkataba wa maelewano na Wizara ya Afya nchini humo.
Akiwa kwenye moja ya interview Eezy amesema kucheleweshwa kwa malipo na kutotimizwa kwa mikataba mingine ambayo wizara ya afya nchini uganda iliahidi ndio imekwamisha juhudi za kuachiwa kwa remix ya wimbo wake wa “Tumbiza Sound.”
Ikumbukwe Wimbo wa “Tumbiza Sound” ni moja kati singles zilizopendwa na wengi kipindi cha lockdown nchini Uganda lakini baadae Wizara ya Afya nchini humo ilikuja ikapiga marufuku wimbo huo kwa madai kwamba inawahimiza watu kwenda kinyume na kanuni za kuthibiti msambao wa corona.
Lakini baadae maafisa katika wazira ya afya nchini uganda walifanya kikao na msanii Eezy ambapo walimuagiza kuachia remix ya wimbo wa “Tumbuiza Sound” kwa ajili ya kuwahimiza watu kufuata taratibu za kuthibiti janga la corona.