NADIA MUKAMI AFIKISHA ZAIDI YA STREAMS MILLIONI 7 KWENYE MTANDAO WA BOOMPLAY.

You are currently viewing NADIA MUKAMI AFIKISHA ZAIDI YA STREAMS MILLIONI 7 KWENYE MTANDAO WA BOOMPLAY.
  • Post category:Burudani

Nyota wa muziki nchini Nadia Mukami anaendelea kupokea upendo na support kubwa kutoka kwa mshabiki wake kiasi cha kufanya vizuri kwenye mtandao wa kusikiliza muziki wa BoomPlay.

Hadi kufikia sasa katika mtandao wa kusikilizia muziki wa Boomplay Nadia Mukami amefikisha wasikilizaji zaidi ya Million 7 kupitia nyimbo zake zote.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Nadia Mukami ambaye anafanya vizuri ha wimbo wake uitwao “Wangu” amewashukuru mashabiki zake  kwa kuendelea kufuatilia kazi zake ambazo zimeonyesha mafanikio makubwa ndani na nje ya nchi.

Kwa mafanikio hayo, Nadia Mukami anakuwa msanii wa kwanza wa kike nchini na wanne katika historia ya muziki nchini kufikisha wasikilizaji Millioni 7 kupitia mtandao huo baada ya Otile Brown, Sauti Sol na Nyanshinski.

Ikumbukwe Nadia Mukami kwa sasa yupo mbioni kuachia album yake mpya mara baada ya EP yake iitwayo “African Popstar” kufanya vizuri kwenye digital platforms zote za kusikiliza na kupakua muziki duniani.

Robert Elim

Robert Elim better known as Mtoto wa Nyumbani Roba is a new shade of light on the mainstream radio scene! He host an Entertainment show called Interact that usually runs every Monday to Friday from 1:00 PM to 4:00 PM and Interact Extra that runs every Saturday from 10:00 AM to 1:00 PM. Follow him on Twitter and Instagram @robertchiwawa