Taharuki imetanda katika kijiji cha Nyawa katika kaunti ndogo ya Keiyo Kaskazini kaunti ya Elgeyo Marakwet baada ya mwanamume mmoja kuvamiwa na kuawa na wanakijiji.
Kulingana na naibu kamishena wa eneo hilo Julius Maiyo, mwendazake alikuwa ameandamana na vijana kutoka kijiji cha Kaptum kwenda kumfuata mke wake hadi nyumbani kwao ambapo wanakijiji walimvamia
Maiyo ameongeza kwamba mwanamme mwingine ambaye alikuwa miongoni mwa vijana hao anauguza majeraha mabaya huku akisema marehemu na mkewe walikuwa na mzozo wa kinyumbani kabla ya mke wake kutorokea nyumbani kwao.