WAKAAZI TURKANA WAHIMIZWA KUUNGA MKONO BBI

You are currently viewing WAKAAZI TURKANA WAHIMIZWA KUUNGA MKONO BBI

Wakaazi wa kaunti ya Turkana wameshauriwa kuunga mkono mchakato wa bbi ili kuleta maendeleo mashinani. 

Akiwahutubia wananchi mjini Kakuma Kinara wa ODM Raila Odinga amesema kuwa BBI ndio njia pekee ya kuhakikisha wakaazi wa kaunti hiyo wamepata maendeleo ikizingatiwa kuwa mgao wa fedha za kaunti utaongezwa kutoka asilimia 15 hadi 35.

Kwa upande wake Mbunge wa Suna Mashariki Junet Mohamed amewataka wakaazi wa Turkana kutopotoshwa na baadhi ya viongozi wanaodai kuwa BBI inaongeza nafasi za uongozi.

Wakati huo mwakilishi wa akina kaunti ya Homabay Gladys Wanga na mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino wamekashifu vikali hatua ya naibu rais kugawa mikokoteni kwa wananchi wakisema hatua hiyo haitabadilisha maisha ya vijana nchini.

Hata hivyo mbunge wa Likoni Mishi Mboko amesema mapendekezo ya ripoti ya BBI itatatua suala la ghasia za baada ya uchaguzi pamoja na kuhakikisha usawa wa uakilishi na ugavi mapato.

Robert Elim

Robert Elim better known as Mtoto wa Nyumbani Roba is a new shade of light on the mainstream radio scene! He host an Entertainment show called Interact that usually runs every Monday to Friday from 1:00 PM to 4:00 PM and Interact Extra that runs every Saturday from 10:00 AM to 1:00 PM. Follow him on Twitter and Instagram @robertchiwawa